Posts

Kuhusu Sisi

Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania ((Tanzania Forest Services (TFS) Agency)) ulianzishwa kisheria kupitia Tangazo la Gazeti la Serikali (GN 269) la tarehe 30/7/2010 na kuzinduliwa rasmi tarehe 18/7/2011. Kuanzishwa kwa Wakala wa Huduma za Misitu ni kwa mujibu wa Sheria ya Wakala “the Executive Agencies Act Cap. 245 (Revised Edition 2009)”, pamoja na Sera ya Misitu ya mwaka 1998, Sera ya Ufugaji Nyuki ya mwaka 1998, Sheria za Misitu na Nyuki Sura 323 na Sura 224 za mwaka 2002. Aidha, Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania uliundwa kwa kuzingatia Programu ya Serikali ya Maboresho katika Utumishi wa Umma ya mwaka 2000 (Public Service Reforms Programme (PSRP 2000)). Programu hii ililenga kuimarisha Idara na Wakala (Ministerial Departments & Agencies (MDAs)) katika kuhakikisha utoaji wa huduma bora na madhubuti katika utumishi wa umma, ambapo Wakala zinakuwa na uwezo, motisha na mbinu za mabadiliko yenye kuleta ufanisi na tija kiutendaji.  1.1 Lengo Kuu la Kuanzishwa Wakala wa Huduma

Forest Regulations 2004

Forest Regulations 2004 II Word by TFS Communications on Scribd

THE FOREST ACT, 2002

Forest Regulations by TFS Communications on Scribd

Forest-Act-2002

Forest Act 2002 by TFS Communications on Scribd

Sheria zingine ambazo Wakala unazitumia kufanikisha utendaji

 Katika kutekeleza majukumu yake, Wakala (TFS) unatekeleza Sheria mbalimbali kama: Sheria ya Usimamizi wa Mazingira Na. 20 ya mwaka 2004, Sheria ya Manunuzi ya Umma ya mwaka 2011, Sheria ya Fedha Na. 14 ya mwaka 2001, Sheria ya Ardhi ya mwaka 1999, pamoja na Sheria ya Ardhi ya Vijiji ya mwaka 1999. Sheria ya Mazingira ya 2004  Sheria hii inaweka misingi ya usimamizi endelevu wa mazingira kwa ajili ya kuhifadhi na kudhibiti uharibifu. Aidha, Sheria inaelekeza utekelezaji wa tathmini ya athari ya mazingira kabla ya kufanya uwekezaji katika misitu chini ya uratibu wa Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira. Sheria ya Manunuzi ya Umma 2011  Katika kuhakikisha kuwepo kwa mfumo wenye ufanisi na uwazi katika manunuzi na usimamizi wa manunuzi, Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania unatekeleza Sheria ya Manunuzi ya Umma ya mwaka 2011 (Public Procurement Act, 2011). Sheria hii inabainisha misingi bora na miongozo inayowezesha Wakala kupata huduma kama vifaa (magari, mitambo) na huduma za u

Muundo wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS)

Image
Kulingana na muundo wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania upo mgawanyiko katika maeneo makuu matatu: Makao Makuu, Kanda na Mashamba ya miti.  Makao makuu inaundwa na menejimenti inayojumuisha Mtendaji Mkuu, Wakurugenzi watatu, Meneja wawili wa Vitengo vya Sheria na ugavi, Mhasibu Mkuu na Mkaguzi Mkuu wa ndani. Menejimenti ya Wakala na baadhi ya watumishi wengine wako katika jengo la Mpingo gorofa ya tatu. Wakala pia una Meneja wa Kanda saba (7) na Mashamba ya miti 18. Vile vile Wakala umeboresha utendaji wake kupitia wilaya; ambapo Meneja wa wilaya 118 wameteuliwa na kupatiwa nyenzo za kazi. Tofauti na Kanda saba za awali za Uenezi na vikosi vya Doria za misitu chini ya Idara; Muundo unaojumuisha Kanda saba za Wakala umeboresha tija katika utendaji kwa kuimarisha uhifadhi na usimamizi wa misitu, ukusanyaji wa mapato, uenezi, na ulinzi wa misitu Mchoro wa Muundo wa Wakala (TFS) Kanda za Wakala na Mashamba ya miti  Wakala una Meneja wa Kanda saba (7). Kanda hizo ni Ma

Sisi ni nani?

Image
Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania ((Tanzania Forest Services (TFS) Agency)) ulianzishwa kisheria kupitia Tangazo la Gazeti la Serikali (GN 269) la tarehe 30/7/2010 na kuzinduliwa rasmi tarehe 18/7/2011. Kuanzishwa kwa Wakala wa Huduma za Misitu ni kwa mujibu wa Sheria ya Wakala “the Executive Agencies Act Cap. 245 (Revised Edition 2009)”, pamoja na Sera ya Misitu ya mwaka 1998, Sera ya Ufugaji Nyuki ya mwaka 1998, Sheria za Misitu na Nyuki Sura 323 na Sura 224 za mwaka 2002. Aidha, Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania uliundwa kwa kuzingatia Programu ya Serikali ya Maboresho katika Utumishi wa Umma ya mwaka 2000 (Public Service Reforms Programme (PSRP 2000)). Programu hii ililenga kuimarisha Idara na Wakala (Ministerial Departments & Agencies (MDAs)) katika kuhakikisha utoaji wa huduma bora na madhubuti katika utumishi wa umma, ambapo Wakala zinakuwa na uwezo, motisha na mbinu za mabadiliko yenye kuleta ufanisi na tija kiutendaji.  1.1 Lengo Kuu la Kuanzishwa Wakala wa Hudum