Posts

Showing posts with the label Home

Kuhusu Sisi

Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania ((Tanzania Forest Services (TFS) Agency)) ulianzishwa kisheria kupitia Tangazo la Gazeti la Serikali (GN 269) la tarehe 30/7/2010 na kuzinduliwa rasmi tarehe 18/7/2011. Kuanzishwa kwa Wakala wa Huduma za Misitu ni kwa mujibu wa Sheria ya Wakala “the Executive Agencies Act Cap. 245 (Revised Edition 2009)”, pamoja na Sera ya Misitu ya mwaka 1998, Sera ya Ufugaji Nyuki ya mwaka 1998, Sheria za Misitu na Nyuki Sura 323 na Sura 224 za mwaka 2002. Aidha, Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania uliundwa kwa kuzingatia Programu ya Serikali ya Maboresho katika Utumishi wa Umma ya mwaka 2000 (Public Service Reforms Programme (PSRP 2000)). Programu hii ililenga kuimarisha Idara na Wakala (Ministerial Departments & Agencies (MDAs)) katika kuhakikisha utoaji wa huduma bora na madhubuti katika utumishi wa umma, ambapo Wakala zinakuwa na uwezo, motisha na mbinu za mabadiliko yenye kuleta ufanisi na tija kiutendaji.  1.1 Lengo Kuu la Kuanzishwa Wakala wa Hu...

SERIKALI YAONYA UNUNUZI WA ARDHI KATIKA HIFADHI YA MSITU WA KAZIMZUMBWI

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Prof. Dos Santos Silayo amewaasa wananchi kutonunua maeneo ya ardhi ndani ya Hifadhi ya Msitu wa Kazimzumbwi yanayouzwa na wavamizi. Akizungumza mwanzoni mwa wiki jijini Dar es Salaam, Prof. Silayo alisema Serikali haijabadili matumizi ya Hifadhi ya Msitu wa Kazimzumbwi ulioko Kisarawe mkoani Pwani , na kwamba eneo hilo lisikaliwe na raia yeyote au kutumika kwa namna nyingine yoyote kama ilivyotanganzwa na tangazo la Serikali Na. 306 lililochapishwa 24/9/54 AN 4/67/20. Aliyazungumza hayo mara baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Mkurugenzi wa Usimamizi Rasilimali za Misitu , Bw. Zawadi Mbwambo kuwa kuna watu wamevamia Hifadhi ya Msitu wa Kazimzumbwi na kuanzisha makazi na wengine wanafanya shughuli nyingine za kibinadamu ikiwemo kuuza viwanja. Alisema kinachofanywa na wavamizi hao ni kinyume na sheria na Serikali haitawavumilia wale wote waliovamia na kuanzisha makazi ndani ya maeneo ya hifadhi ya msitu na hi...