Kulingana na muundo wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania upo
mgawanyiko katika maeneo makuu matatu: Makao Makuu, Kanda na Mashamba ya miti.
Makao makuu inaundwa na menejimenti inayojumuisha Mtendaji Mkuu, Wakurugenzi
watatu, Meneja wawili wa Vitengo vya Sheria na ugavi, Mhasibu Mkuu na Mkaguzi Mkuu
wa ndani. Menejimenti ya Wakala na baadhi ya watumishi wengine wako katika jengo
la Mpingo gorofa ya tatu.
Wakala pia una Meneja wa Kanda saba (7) na Mashamba ya
miti 18. Vile vile Wakala umeboresha utendaji wake kupitia wilaya; ambapo Meneja wa
wilaya 118 wameteuliwa na kupatiwa nyenzo za kazi. Tofauti na Kanda saba za awali za
Uenezi na vikosi vya Doria za misitu chini ya Idara; Muundo unaojumuisha Kanda saba za
Wakala umeboresha tija katika utendaji kwa kuimarisha uhifadhi na usimamizi wa misitu,
ukusanyaji wa mapato, uenezi, na ulinzi wa misitu
Mchoro wa Muundo wa Wakala (TFS)
Kanda za Wakala na Mashamba ya miti
Wakala una Meneja wa Kanda saba (7). Kanda hizo ni Mashariki, Kaskazini, Kati, Kusini,
Nyanda za juu Kusini, Ziwa na Magharibi. Vile vile Wakala umeimarisha utendaji katika
ngazi ya Wilaya kwa kuteua na kusambaza Meneja wa Wilaya 118. Aidha katika ofisi 6 za
kanda, Wakala unatumia majengo yaliyokuwa ya FBD ambayo yamefanyiwa ukarabati ili
yaweze kutumika. Katika kanda ya Kusini, Wakala umekodi nyumba mjini Masasi. Aidha,
wapo Meneja wa mashamba ya miti 18 ambayo ni: Buhindi, Kawetire, Kiwira, Korogwe,
Longuza, Mbizi, Meru, Mtibwa, Kilimanjaro Kaskazini, Kilimanjaro Magharibi, Ruvu
Kaskazini, Rondo, Rubare, Rubya, Sao Hill, Shume Ukaguru na Wini-Ifi nga. Meneja
wa mashamba ya miti 15 wanatumia majengo yaliyokuwa chini ya FBD. Meneja wa
Mashamba mapya wanatumia majengo yaliyopangishwa kwa Wakala au ofi si za zamani za
idara ya misitu zilizotolewa na Halmashauri za Wilaya husika. Kila Meneja wa Kanda na
wa shamba wana vitendea kazi kama magari, pikipiki, mitambo, kompyuta za vipakatalishi
na mezani pamoja na vifaa vingine muhimu vya ofi si kwa ajili ya kufanyia kazi za Wakala.
Pamoja na vitendea kazi kuwa vichakavu, kila Meneja ana bajeti ambayo iko kwenye
mpango kazi wa kibiashara ukianisha shughuli za Wakala katika ngazi hiyo mfano,
ukarabati wa majengo, barabara na ununuzi wa vitendea kazi; kama vile magari, pikipiki
na matumizi mengine.
Majengo na vitendea kazi yaliyokuwa ya FBD yote yamechukuliwa na Wakala (TFS) na
kwa sasa ni mali ya TFS. Hali ya majengo yote yanayotumika ni nzuri kwa vile yanafanyiwa
ukarabati mara kwa mara. Aidha, Wakala una mpango wa kujenga majengo ya vitega
uchumi katika miji ya Mbeya, Kibaha na Dar es Salaam. Hii ni pamoja na kukaratiba
majengo ambayo yalikuwa chini ya FBD ambayo kwa sasa hayatumiki ili kuweza kutumika
kama vitega uchumi vya Wakala. Majengo hayo yapo miji ya Morogoro, Moshi, Tanga na
Shinyanga.
Mifumo ya Utendaji ya Wakala
Baada ya Kuanzishwa
Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania umeweka mifumo mbalimbali ya kimenejimenti
kwa malengo ya kuongeza ufanisi wa kiutendaji, kuboresha utoaji huduma kwa wananchi
na kupunguza gharama za uendeshaji wa shughuli za Wakala. Kwa sehemu kubwa Mifumo
hii inaratibiwa na Kurugenzi ya Huduma na Uendeshaji Shughuli katika Wakala. Mifumo
hii ni pamoja na Mwongozo wa Utendaji Kazi, Hati ya Kuanzisha Wakala, Mpango
Mkakati, Mpango wa Biashara wa Mwaka, Mfumo wa Wazi wa Mapitio na Tathmini ya
Utendaji Kazi (OPRAS), Uperembaji na Tathmini, Mkataba wa Huduma kwa Mteja na
Mfumo wa Kushughulikia Malalamiko. Aidha mifumo mingine inayotumiwa na Wakala
kutekeleza majukumu yake ni Mfumo wa usimamizi na uhakiki wa fedha (Integrated
Financial Management System (IFMS)), Human Capital Information Management
System, Masjala na Uhasibu.
Can I get a chance to work with you as a accountant manager????
ReplyDeleteMshaara Wa mtu mwenye diploma ya misitu ni shingapi
ReplyDelete