Kuhusu Sisi

Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania ((Tanzania Forest Services (TFS) Agency)) ulianzishwa kisheria kupitia Tangazo la Gazeti la Serikali (GN 269) la tarehe 30/7/2010 na kuzinduliwa rasmi tarehe 18/7/2011. Kuanzishwa kwa Wakala wa Huduma za Misitu ni kwa mujibu wa Sheria ya Wakala “the Executive Agencies Act Cap. 245 (Revised Edition 2009)”, pamoja na Sera ya Misitu ya mwaka 1998, Sera ya Ufugaji Nyuki ya mwaka 1998, Sheria za Misitu na Nyuki Sura 323 na Sura 224 za mwaka 2002. Aidha, Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania uliundwa kwa kuzingatia Programu ya Serikali ya Maboresho katika Utumishi wa Umma ya mwaka 2000 (Public Service Reforms Programme (PSRP 2000)). Programu hii ililenga kuimarisha Idara na Wakala (Ministerial Departments & Agencies (MDAs)) katika kuhakikisha utoaji wa huduma bora na madhubuti katika utumishi wa umma, ambapo Wakala zinakuwa na uwezo, motisha na mbinu za mabadiliko yenye kuleta ufanisi na tija kiutendaji.  1.1 Lengo Kuu la Kuanzishwa Wakala wa Huduma

Sheria zingine ambazo Wakala unazitumia kufanikisha utendaji

 Katika kutekeleza majukumu yake, Wakala (TFS) unatekeleza Sheria mbalimbali kama: Sheria ya Usimamizi wa Mazingira Na. 20 ya mwaka 2004, Sheria ya Manunuzi ya Umma ya mwaka 2011, Sheria ya Fedha Na. 14 ya mwaka 2001, Sheria ya Ardhi ya mwaka 1999, pamoja na Sheria ya Ardhi ya Vijiji ya mwaka 1999.

Sheria ya Mazingira ya 2004 
Sheria hii inaweka misingi ya usimamizi endelevu wa mazingira kwa ajili ya kuhifadhi na kudhibiti uharibifu. Aidha, Sheria inaelekeza utekelezaji wa tathmini ya athari ya mazingira kabla ya kufanya uwekezaji katika misitu chini ya uratibu wa Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira.

Sheria ya Manunuzi ya Umma 2011 
Katika kuhakikisha kuwepo kwa mfumo wenye ufanisi na uwazi katika manunuzi na usimamizi wa manunuzi, Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania unatekeleza Sheria ya Manunuzi ya Umma ya mwaka 2011 (Public Procurement Act, 2011). Sheria hii inabainisha misingi bora na miongozo inayowezesha Wakala kupata huduma kama vifaa (magari, mitambo) na huduma za ujenzi wa miundombinu mbalimbali kulingana na thamani halisi ya fedha.

Sheria ya Fedha 2001
Sheria hii (Finance Act 2001) inaweka misingi ya kudhibiti Kodi na mapato ya Serikali kwa nia ya kuongeza makusanyo (mapato ya Serikali). Wakala wa Huduma za Misitu umekuwa mstari wa mbele katika makusanyo ya Serikali hususan Kodi ya ongezeko la thamani (Value Added Tax - VAT).

Sheria ya Ardhi 1999 na Sheria ya Ardhi ya Vijiji 1999 
Sheria hizi zinaweka misingi kwa Vijiji kumiliki na kusimamia rasilimali za misitu katika ardhi ya Kijiji na kuzitumia katika misingi endelevu kwa kutengeneza na kusimamia Sheria ndogo kupitia Kamati za Maliasili (Village Natural Resources Committees – VNRCs)) na mpango wa Usimamizi Shirikishi wa Misitu (Participatory Forest Management – PFM).

Comments

  1. Harrah's Casino & Hotel in Atlantic City - Mapyro
    View 제주도 출장마사지 Harrah's Casino & 울산광역 출장안마 Hotel (Harrah's Casino & 인천광역 출장안마 Hotel) location in Atlantic City, NJ, revenue, industry 문경 출장샵 and 서귀포 출장샵

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

Muundo wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS)

Kuhusu Sisi